Maelezo kwa Watafiti na Waandishi

Umetoholewa toka kijitabu cha KAWAKIA “Maelezo kwa Watafiti na Waandishi”*

1.Majina ya kupewa ya mhusika. Ikibidi toa maelezo ya maana ya majina hayo.

  • Majina ya ubatizo
  • Majina ya ukoo
  • Majina ya utani

2. Majina ya kifamilia. Ikitokea kuna zaidi ya mume/mke mmoja, orodhesha watoto chini ya mama au baba husika.

  • Baba
  • Mama
  • Mke / Wake
  • Mume / Waume
  • Watoto
  • Wajukuu 3. Kikundi cha jadi - lugha na kikundi cha ukoo

4. Matukio maishani

  • Tarehe au tarehe ya karibu ya kuzaliwa
  • Mahali pa kuzaliwa: Kijiji, Mji, Mkoa, Taifa
  • Matukio yasiyo ya kawaida kuhusiana na kuzaliwa
  • Majaribu maishani, kama vile magonjwa, mikasa binafsi, majanga, na maono
  • Elimu, shahada (pamoja na tarehe)
  • Kuingia ukristo (pamoja na tarehe, kama inafaa)
  • Wito na / au kuwekwa wakfu kwa utumishi wa Bwana (pamoja na tarehe, kama inafaa)
  • Tarehe, mahali na mazingira ya kifo

5. Utaifa / Uraia

6. Lugha, pamoja na ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne, ya tano, n.k.

7. Madhebu ya kanisa lake

  • Katoliki
  • Orthodox, Coptic
  • Protestanti (Conciliar, Kiinjilisti, Anabatisti)
  • Huru (Africa - initiated, Kiroho, Pentekoste / Karismatiki)

8. Majina, mahali, na maelezo ya makanisa yaliyoasisiwa na kuhudumiwa na mhusika

9. Utumishi wa Bwana kwa kina. Wapi? Kwa muda gani? Kulitokea nini? Adhari ya muda mfupi na mrefu?

  • Tafadhali toa taarifa kamili kila inapowezekana, ikiwa ni pamoja na michapo, hadithi, na tetesi

10. Ushawishi na umaarufu unaoendelea wa mhusika

11. Vitabu, ripoti, maandiko, barua, tunzi za nyimbo, na sanaa kazi ya mhusika

12. Vyanzo vya taarifa kumhusu mhusika

Vyanzo visivyochapishwa - Simulizi za ushahidi wa macho (toa majina na anwani za wasimulizi ambao ni au walikuwa mashahidi wa macho, na jumuisha taarifa za kina za uhusiano wao na mhusika). Simulizi nyingine za mdomo na hadithi fupi (taja majina na anwani za wasimulizi kila inapowezekana, na jumuisha kikamilifu uhusiano na mhusika)

Vyanzo vilivyochapishwa - Kila inapowezekana jumuisha habari kamili za bibliografia:

  • Mtunzi wa kitabu, jina la kitabu, mahali, mchapishaji na mwaka wa kuchapishwa
  • Mtunzi wa sura katika kitabu, jina la sura, jina la kitabu, jina la mhariri wa kitabu, habari kamili za uchapishaji * Mtunzi wa makala ndani ya jarida, jina la makala, jina la jarida, juzuu na namba ya jarida tarehe ya jarida, namba za kurasa za makala

13. Taarifa nyingine yoyote inayofaa.

Ili kukupa sifa unayostahili kama mchangiaji, tafadhali jumuisha:

  • Jina lako na anwani.
  • Jina na anwani ya kanisa lako.
  • Jina na anwani ya taasisi ya elimu au wakala wa misheni (Taasisi shiriki).
  • Jina (majina) la mtu (watu) aliyehusika hasa kutafiti hadithi ya kila somo.
  • Jina na cheo cha msimamizi wa utafiti.
  • Tarehe ya kuwasilisha hadithi.

Kamusi ya Wasifu wa Wakristo wa Kiafrika
Center for Global Christianity and Mission (CGCM)
745 Commonwealth Avenue
Boston, Massachussetts 02215, USA
Email: [email protected]