Bure Ukusanyaji wa KAWAKIA

Vifungu vyote viliunda au kuwasilishwa wakati wa miaka ishirini ya kwanza ya mradi huo, kutoka 1995 hadi 2015.

Sarikas, Nikodemos

1878-1941
Kanisa la Orthodox la Kigiriki
Tanzania

Nikodemos Sarikas alizaliwa Uturuki, na alikuwa mtawa wa kiume katika umri wa miaka 17. Alikaa na Baba Damaios mjini Jerusalemu, akafanywa kasisi Smyrna katika mwaka 1907 (Mantzaris sa).

Mwaka 1907 alienda Johannesburg, na alifanywa kasisi wa kwanza wa Kanisa la Kigiriki la Othodoksi kwenye sehemu ya Transvaal. Alikuwa na huzuni pale kwa sababu wanaparokia walitaka kumfungia dhehebu lake kwa wanachama wa umma wa Kigiriki, nao hawakumtaka kufanya kazi ya misheni. Mwaka 1911 alihamia wilaya ya Moshi katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika) na kuwa mkulima.

Sarikas alitembelea Uganda mwaka 1933 kwa sababu ya mwaliko wa Reuben Spartas, ambaye alikuwa amemfanywa kasisi kwenye Kanisa la Othodoksi la Kiafrika na Daniel William Alexander. Isitoshe, alionana mara kwa mara na viongizi wa Kanisa la Othodoksi la Kiafrika katika sehemu ya Kikuyu, Kenya. Alimtumia barua Askofu wa Alexandria kumwuliza kwamba amsaidie kuchukua Kanisa la Othodoksi la Kiafrika chini ya utunzi wake. Aliwachukua Waganda wawili kuwarudisha Moshi kuishi naye, na akawafundisha juu ya Kanisa la Othodoksi. Kwa njia hii, Sarikas alianzisha uhusiano wa kirafiki baina ya kanisa la Spartas na umma wa Kigiriki mjini Kampala (Welbourn 1961:89).

Stephen Hayes


Bibliographia:

Mantzaris, E. Mswada ambao haujachapishwa.

Welbourn, F. B. 1961. East African Rebels: A Study of Some Independent Churches. London: SCM.


Makala haya yametokana na Database of African Church Leaders, ambayo ni sehemu ya Database of African Independent Churches zinahifadhiwa na Stephen Hayes. Haki zote zimehifhadiwa.