Machozi, Vincent

1965 - 2016 Kanisa Katoliki
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo


Tarehe 20 mwezi wa tatu, mwaka 2016, Machozi, padri Mtwaliwa au Padre wa Assumption, alipigwa risasi na kuuawa na kundi la waasi kijijini Katolu, karibu na mji wa Butembo, jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alikuwa na umri wa miaka 51. Machozi aliuawa alipokuwa barazani katika kituo cha kijamii ambako mikutano ya kuleta amani kati ya wakuu wa Kinande ilikuwa ikiendelea. Maneno yake ya mwisho yalikuwa: “mbona unaniua?” Alishapokea vitisho na aliweza kutoroka majaribio mengine kadhaa ya kumwua.

Machozi aliongoza tovuti alipochapisha habari kuhusu vita na mauaji katika jimbo lake la Kivu Kaskazini ili kuunga mkono na watu wa kawaida walioteseka kwa ajili ya vurugu hizo. Machozi aliuawa baada ya kuchapisha makala iliyomhusisha rais wa Kongo Joseph Kabila katika vurugu na fujo zilizoua watu wengi katika sehemu ya Beni-Butembo tangu mwaka 2014.

Machozi alitoka katika familia yenye watoto 13, baadhi yao walifariki wangali watoto wadogo. Kwa sababu ya vifo vya ndugu zake, alipewa jina la mwisho wa Machozi. Safari yake ya kiroho na the Assumptionist Order ilianza alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba. Machozi alikuwa Mnande na aliongea Kinande, Kiswahili, Kilingala, Kifaransa, na Kiingereza.

Alipata shahada kadhaa zikiwemo shahada ya pili ya Theolojia kutoka shule ya Theolojia katika Chuo Kikuu cha Boston. Wakati fulani aliamua kufupisha masomo yake kwasababu alisikia wito kurudi nyumbani kuendelea kazi yake ya harakati za kutetea haki za binadamu nchini Kongo. Profesa Dana Robert, ambaye ni Profesa wa Dini ya Kikristo Duniani katika Chuo Kikuu cha Boston, alisifu kazi na maisha ya mwanafunzi wake wa zamani kama mkristo katika hali ya ushahidi, alisema: “kuwapa sauti wale wasio na sauti,” Alitoa uhai wake kama sadaka kwa ajili ya wito huu.


Marejeleo:
“Watu wenye bunduki wamuua Padri wa Kongo aliyeripoti juu ya ukatili,” Catholic News Agency, ilipatikana Tarehe 29 Machi, 2016.
“Mauaji ya Padri nchini Kongo yaonyesha mahitaji ya dhana mpya ya kufia imani,” Crux, na John Allen, ilipatikana Tarehe Machi 29, 2016.
“Mapadri wa kundi la Watwaliwa wa Marekani au USA Assumptionist Wamkumbuka Father Vincent Machozi kama “Mfiadini wa Ukweli”,, Beni Lubero Online, Ilisomwa tarehe 31 Machi, 2016. “Padri Mtwaliwa wa Kikongo Auawa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo” BU Today, Ilipatikana Tarehe 16, Aprili, 2019. “Fr. Vincent Machosi”


Ilitafsiriwa na Joshua Castillo, mwanafunzi wa darasa la Kiswahili (kiwango cha juu) linalofundishwa na Mwl. Judith Mmari, Mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Boston.